October 6, 2010
Inspired by real events...
Ndani ya Dakika kumi
Raha imeisha
Utamu umeondoka
Na ukweli umekuja
Hali halisi ya majuto.
Ndani ya dakika kumi,
Nimetoa nguvu zangu,
Nimemdhalilisha Mungu wangu
Nimeingia hasara kubwa,
Nimewapa sifa hawa mbwa!
Ndani ya dakika kumi
Sioni tena ile thamani
Niliyokuwa nayo hapo zamani
Kubadili matukio natamani
Inaumiza moyo hii tafrani!!
Ndani ya dakika kumi
Ningeweza kusema hapana
Kuondokana na hii laana
Ningeweza tangaza msimamo
Kuchagua kuishi kama mfano
Ndani ya dakika kumi
Ningeweza zuia huu ujauzito
Nisingepitia haya mapito
Laiti mapema ningetiliia maanani
Historia ingekua tofauti jamani
Ndani ya dakika kumi
Ningeishinda nafsi yangu
Ningeipa nguvu roho yangu
Ningemfurahisha Bwana wangu
Kwa kutotimiza starehe za hisia zangu
Ndani ya dakika kumi
Akili imenijia
Toba imenitawala
Najua mwili una muumba
Hilo halina mjadala
Ndani ya dakika kumi
Ninaamua kumpa nafasi
Yeye Mkuu aliyeamua kukaa nasi
Kwa nguvu zangu sitaweza
Nakiri yeye ndiye muweza
Ndani ya dakika kumi
Ninatambua sio uamuzi wa siku moja
Badiliko litachukua zaidi ya dakika kumi
Lakini mradi na Mungu tupo pamoja
Niko tayari aniongoze kila dakika kumi!
Nimeipenda hii poem, Ndani ya dakika kumi
ReplyDelete